Tuesday, 14 April 2015

ETOILE YAIVUTIA PUMZI YANGA..

Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia inatarajiwa kuwasili Dar es Salaam wiki hii kwa ajili ya mechi yao ya kukata na shoka dhidi ya Yanga katika kombe la vilabu la Shirikisho barani Afrika.
Habari kutoka Yanga zinasema wapinzani wao wanaweza kutinga Dar es Salaam kati ya Alhamisi au Ijumaa kwa mechi ya kwanza itakayochezwa kati ya April 17 au 18 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi ya marudiano itachezwa Tunis, Tunisia baada ya wiki mbili.
Yaanza imeanza kuwavutia kasi wapinzani wao kufuatia wimbi la ushindi katika mechi zake za Ligi kuu.
Katika mechi za hivi karibuni, mabingwa hao wa zamani waliweka historia ya mvua ya magoli katika msimu baada kwa kuipa Coastal Union kichapo cha 8-0 na baadae Mbeya City 3-1 na kujikita kileleni ikiwa name pointi 46.
Tayari kocha wa Yanga, Hans Pluijm amewaonya wachezaji wake kuwa makini na kuweka akilini kuwa watakutana na moja ya timu ngumu barani Afrika katika hatua ya 16 bora .
Yanga iliwatoa Wazimbabwe, Platinum FC na sasa itatumia mechi zake za ligi kuu kama sehemu ya mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo muhimu.

MASKINI.....WEMA,AZOMEWA LICHA YA KUJIELEZA.

Muigizaji maarafu wa filamu nchini Tanzania,Wema Sepetu alizomewa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram
baada ya kuweka picha ya mlimbwende Hamisa Obetto akiwa mjamzito na kuandika maneno ya mshangao
”Jamani my mdogo umezaa.!wewe ni mwanamke sasa”.
Ujumbe huo ulizusha tafrani kwa baadhi ya watu na kumjibu Wema kwa maneno makali yenye kebehi ya
kwa nini yeye hazai anakaa kushabikia watoto wa wenzie tu.
Gumzo hilo lilifwata mkondo tofauti pale ambapo mchumba wake wa zamani mwanamuziki Diamond Platinum
akitarajia kupata mtoto na bi.Zari kutoka Uganda ambaye ni mpinzani wake mkubwa Wema.
Wema Sepetu aliweza kujibu tuhuma hizo kwa kusema yeye si mpanga wa yote,''ningekuwa na uwezo wa kuzaa angezaa siku nyingi ila ni Mungu ndiye anapanga'',
Alisema kuwa ''nimekuwa nikihangaika kupata mtoto usiku na mchana''
aliongezea kusema kuwa si rahisi kwa yeye kuwaambia kila kitu,kwani yeye pia ni binadamu na kuwa
''anaumia sana na maneno makali watu wanayoandika au kusema kumhusu''.
Ujumbe wa simanzi kutoka kwa muigizaji huyo ulirudiwa na baadhi ya waigizaji kama Iren Uwoya na mashabiki wengine
ukionya tabia ya watu kutoa matusi makali kwa Wema bila kuangalia upande wa pili,maana siku hizi kuna team kwenye mtandao pia zikijiita team Wema na Team Zari

Wednesday, 8 April 2015

HII SASA NI SIFA...YANGA YAIFUMUA COASTAL 8

Yanga hii ni ya kimataifa na kitaifa ndiyo habari ya mjini Coastal Union hawatasahau milele kipigo cha jana tarehe 8 mwezi wa 4 wapigwa bao sawa na tarehe ya siku ya mchezo wao na Yanga taifa. Amis Tambwe apiga nne, Mliberia  nae afunga bao lake la kwanza toka ajiunge Yanga na baada ya kufunga bao hilo alitoa machozi kwa furaha pia mliberia huyo alitoa pasi tatu zilizo zaa mabao matatu katika mchezo huo. Yanga sasa inazidi kujikita kileleni kwa kuwa na point 43 wakishuka dimbani mara 20, Azam baada ya kukabwa koo leo na Mbeya City kwa kufungana bao 1 kwa 1 wamebakia na point 37 baada ya kushuka dimbani mara 19. Wafungaji wa mabao  Tambwe nne, Msuva mbili Mliberia moja na Telela moja.
Hadi mwisho wa mchezo Yanga 8 na Coastal Union 0.

Saturday, 31 January 2015

COSTA APIGWA STOP MECHI TATU.

Mchezaji wa Chelsea Diego Costa amepigwa marufuku ya mechi tatu kwa kumkanyaga makusudi mchezaji wa Liverpool Emre Can.
Costa mwenye umri wa miaka 26 atakosa mechi ya wikendi dhidi ya Mancity pamoja na mechi dhidi ya Aston Villa na Everton.
Shtaka hilo ambalo Costa alilikana linatokana na kisa cha mchuano wa kombe la leage Cup raundi ya pili ambapo Chelsea iliibuka kidedea.
Costa aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni millioni 32 ana mabao 17 katika mechi 19 za ligi ya Uingereza msimu huu.
Kisa hicho hakikuonekana na maafisa waliosimamia mechi hiyo lakini kilionekana katika kanda ya video.

Saturday, 24 January 2015

RAIS KIKWETE APANGUA BARAZA LA MAWAZIRI.

Rais Jakaya kikwete ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano.
Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene
Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga ya taifa moja kwa moja.
Hii ndio orodha ya mawaziri walioteuliwa
MAWAZIRI
George Simachawene waziri wa nishati na madini
Mary Nagu- waziri wa nchi [afisi ya rais] mahusiano na uratibu
Christopher chiza -waziri uwezeshaji na uwekezaji
Harisson Mwakyembe[waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki]
William Lukuvi -waziri wa ardhi nyumba na makaazi
Steven Wasira -waziri wa kilimo chakula na ushirika
Samwel Sita -waziri wa uchukuzi
Jenista Muhagama -waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge
MANAIBU WAZIRI
Stephen Masele -naibu waziri afisi ya makamu wa rais muungano
Angela Kariuki -naibu waziri wa ardhi nyumba na makaazi
Ummi Mwalimu- naibu waziri wa katiba na sheria
Anna Kilango naibu waziri wa elimu na mafunzo ya kiufundi
Charles Mwijage-naibu waziri wa nishati na madini

BREAKING NEWS....WAZIRI MUONGO AACHIA NGAZI..

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muongo ametangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na Sakata lililokuwa linaendelea la Escrow ambapo yeye kama waziri anatuhumiwa kwa rushwa.
Katika uamuzi wake huo,Prof. Muongo ameendelea kusisitiza kuwa yeye ni mtu safi na kwamba yeyote mwenye ushahidi na tuhuma dhidi yake ajitokeze na kuziweka hadharani.

DUU,Hebu sikia hii.......

Je unakumbuka kisa cha wapenzi wawili waliozua gumzo nchini Kenya?

Msichana mhindi Sarika Patel kutoka familia tajiri na Timothy Khamala mbukusu kutoka familia maskini kutoka Magharibi mwa Kenya kuoana? wakati yao mapenzi yao yalijulikana kama Bukusu Darling, sifa kwa wanakoishi wawili hao.
Taarifa sasa ni kwamba mapenzi yao yamefika kikomo. Familia ya msichana Sarika ililaani sana mapenzi hayo kwani Timothy alikuwa anafanya kazi kwao kama mfanyakazi wa nyumbani.
Na Sarika alipoamua kwenda kuishi na Timothy kama mume na mke familia yake ilimfukuza na kisha kumfuta kazi Timothy.
Wawili hao walioana kinyume na matakwa ya familia ya Sarika ambayo kwao ilikuwa ni kama aibu kubwa sana kwa mtoto wao kutoka familia tajiri kuolea na kijana asiyekuwa na mbele wala nyuma.
Wakati taarifa ya wawili hao ilipogonga vichwa vya habari nchini Kenya, Sarika na mume wake walipata kazi katika kiwanda cha kutengeza Sukari kutoka kwa wahisani.
Lakini sasa kuna madai kwamba ndoa yao imevunjika baada ya Sarika kulalamika kwamba Timothy amekuwa akimdhulumu na kumtusi kila mara hali iliyosababisha wawili hao kutalakiana.
Mtandao wa Standard Digital umemnukuu Sarika akisema: "nilipokuwa mgonjwa , hakuwa hata na muda wa kunipeleka hospitalini badala yake wazazi wake ndio walionipeleka kutafuta matibabu. Mbali na hayo amekuwa akinichapa, '' alisema Sarika huku akibubujikwa na machozi.
Kwa sasa inaarifiwa anajuta sana kwa nini alikaidi amri ya wazazi wake.
''Ninajuta sana kwa nini sikuwasikiliza wazazi wangu na kuolewa kinyume na mapenzi yao. Ninaomba radhi, natumai watanikubali kurejea nyumbani. ''
Sarika ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano, ameamua kurejea nyumbani na kusema kamwe hatawahi kuwa na uhusiano wa kimepenzi tena. Lakini wazazi wake wamempa masharti, mwanzo aishi na rafiki yake huku akifanya uamuzi wa mwisho kuhusu anakotaka kuishi.
Anasema anahofia kwamba jamii ya wahindi haitamkubali tena kwani hakuwasikiliza wakati walipomshauri kutoolewa na mwanamume mwafrika.

Friday, 23 January 2015

EEEH,EBU SIKIA HII YA MASOGANGE!!

MIEZI michache tangu ahamishie makazi yake nchini Afrika Kusini, modo aliyetikisa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametia aibu kutokana na kudaiwa ‘kujiuza’ kwa njia ya mtandao nchini humo.
Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza ubuyu kuwa, Masogange yupoyupo tu, kazi kujipiga picha za utupu na kuzitupia mtandaoni kana kwamba anatafuta wanaume.“Kimsingi hana kazi huku Sauz zaidi ya kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram na anachanganya sana wanaume wenye pesa zao, si unajua tena mtoto kajaliwa shepu la maana.
“Ukitaka kuthibitisha hilo ninalokwambia, ingia katika akaunti yake utaona picha kibao za kihasara akiwa hotelini, kama siyo kutuaibisha na kujiaibisha mwenyewe ni nini?” kilihoji chanzo chetu.

Baada ya chanzo hicho kuvujisha ubuyu huo, paparazi wetu aliingia kwenye akaunti ya mrembo huyo na kujionea picha kibao zenye mapozi ya kihasara. Jitihada za kumpata ili azungumzie madai hayo hazikuzaa matunda kwani simu yake haikuwa hewani lakini katika maelezo yake kwenye mitandao ya kijamii amewahi kudai anasoma chuo ingawa haijajulikana ni chuo gani.

Thursday, 22 January 2015

WHATSAPP YAWABANA WATUMIAJI WAKE.

Mtandao wa kijamii wa WhatsApp unawabana watu wanaotumia huduma hio kupitia programu bandia na ambayo haijaidhinishwa ya Android kwa muda wa saa 24.
WhatsApp ambayo inamilikiwa na Facebook, ilisema kuwa imechukua hatua dhidi ya watumiaji wa huduma ya WhatsApp Plus kwa sababu ya wasiwasi kwamba programu hiiyo huenda iksababisha kuvuja kwa taarifa za siri za watumiaji wa WhatsApp.
Programu hio bandia na isio rasmi ya Android inawezesha watumiaji wa WhatsApp Plus kupamba mawasiliano yao wanavyotaka.
Wataalamu wanasema kwamba watumiaji wa Android wanapaswa kuwa makini na kutahadhari kuhusu wanavyodownload programu flani au 'Apps'.
Mtandao wa WhatsApp ulisema hivi karibuni kwamba ina watumiaji milioni 700 wanaotuma ujumbe bilioni 30 kila siku. Kwa sasa inatoza dola 0.99 kwa watumiaji wake wanaotumia huduma ya WhatsApp Plus kila mwaka.
''Lengo letu ni kuhakikisha kwamba huduma ya WhatsApp ni ya kasi kwa wanaoitumia, hilo ndio jambo muhimu sana kwetu,'' alisema msemaji wa kampuni hio.
''Watu wengine wamebuni progarmu ambazo bado hazijaidhinishwa na sasa wanazitumia na WhatsApp , kitu ambacho kinaweza kusababisha kupotea kwa ujumbe au baadhi ya taarifa kuvujishwa. ''
''Bila shaka jambo hili linakwenda kinyume na malengo yetu ya kutoa huduma kwa wateja wetu. Kuanzia leo tutaanza kuchukua hatua kali dhidi ya wanaotumia programu ambazo hazijaithinishwa ili kuweza kutumia programu zetu na pia kuwatahadharisha wanaozitumia programu hizo''.
Kulingana na moja ya maduka ya kuuza programu za kwenye mitandao, programu ya WhatsApp Plus yenyewe ilikuwa imekuwa dowloaded mara milioni 35

Sunday, 18 January 2015

CAMERON APINGANA NA PAPA.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amepinga matamshi ya Papa ya juma lilopita aliposema kuwa siyo sawa kufanya mzaha juu ya imani ya watu wengine.
Akijibu kuhusu mashambulio yaliyofanywa na wapiganaji Waislamu dhidi ya gazeti la Ufaransa la Charlie Hebdo, Papa alisema iwapo mtu atamtusi mama ake, ataraji ngumi.
Bwana Cameron hata hivyo alisema katika nchi huru kuna haki ya kukera kuhusu dini ya mtu mwengine.
Aliliambia shirika la habari la CBS la Marekani, kwamba vyombo vya habari vinafaa kuweza kuchapisha vitu ambavyo vinawakera baadhi ya watu - ikiwa siyo kinyume na sheria.

Saturday, 17 January 2015

KIVUMBI CHA AFCON KUANZA RASMI LEO..

Timu kutoka kote Afrika zimewasili nchini Equatorial Guinea wakati ambapo mechi za taifa bingwa barani zitarajiwa kung'oa nanga hii leo ikiwa ni miezi miwili tangu taifa hilo la afrika ya kati likubali kuandaa mechi hizo.
Morocco ndiyo iliokuwa iandae kombe hilo lakini badala yake ikaomba kuahirishwa kwake kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.
Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF hata hivyo lilikataa ombi hilo la Morocco
Mkuu wa CAF (Hicham El Amrani) anasema kuwa kila tahadhari imechukuliwa nchini Equatorial Guinea kuwalinda watu kutokana na ugonjwa wa ebola.
Mechi ya kwanza itakuwa kati ya wenyeji Equatorial Guinea na Congo.

Friday, 16 January 2015

SAKATA LA ESCROW,WENGINE ZAIDI KORTINI.

Dar es Salaam. Meneja Misamaha ya Kodi TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa ,  Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco,  Steven Roman Urassa  na  Mkurugenzi wa fedha BOT , Julius  Rutta  Angello wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa ya mamilioni ya fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.

Watuhumiwa hao wanafanya idadi ya waliofikishwa mahakamani kwa kashfa ya miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow kufikia watano baada ya watumishi wengine wawili wa umma kufikishwa mahakamani hapo Jumatano iliyopita.

Waliofikishwa mahakamani hapo ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma aliwekewa kiasi cha Sh323 milioni kupitia akaunti yake namba 00120102602001.

Mwingine ni Mhandisi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), Wizara ya Nishati na Madini, Theophillo Bwakea aliyepokea rushwa ya Sh161,700,000 kupitia akaunti yake namba 004101102643901.

Mahakama ya Kisutu leo

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa  kinyume na kifungu cha 15 (1)(a) cha sheria ya kupambana na rushwa  namba 11 ya mwaka 2015, walifikishwa  kwa mahakimu wawili tofauti, Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda na Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka.

Akisoma hati ya mashtaka katika kesi namba 16 ya 2015 inayomkabili Kyabukoba,   Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai   alidai mbele ya Hakimu Kaluyenda kuwa Januari 27, 2014 katika Benki ya Mkombozi  wilaya ya Ilala , alipokea Sh1.6 bilioni kupitia akaunti namba 00110202613801.

Swai alidai  kuwa mshtakiwa huyo akiwa katika Benki ya Mkombozi alijipatia kiasi hicho cha fedha  ambacho ni  sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow na kwamba alizipokea kutoka kwa James Burchard Rugemalira  ambaye ni Mshauri huru wa Kitaalam, Mkurugenzi wa VIP Engineering na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni ya  Mabibo Beer Wines and Spirits ambayo ni mali  ya Rugemalira  mahakamani  kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

Alidai kuwa Julai 15, 2015, mshtakiwa huyo Kyabukoba  akiwa  katika benki hiyo ya Mkombozi alipokea rushwa ya Sh161.7 milioni, Agosti 26,2014 alipokea tena rushwa ya Sh 161.7 milioni na  Novemba 14, 2014 alijipatia rushwa ya kiasi kingine cha fedha cha Sh161.7 milioni kupitia kwenye akaunti hiyo, kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni hiyo ya  Rugemalira mahakamani kitu ambacho ni kinyume cha sheria na kwamba  fedha zote hizo ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Kyabukoba aliyakana na upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekwisha kamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali (PH).